Subscribe:

Friday, February 27, 2015

UKISTAAJABU YA MUSA UTAONA YA MWALIMU WA SAYANSI ANAYEISHI NA LUNDO LA KINYE NA MIKOJO NDANI YA CHUMBA CHAKE

Kinyesi kilichokutwa ndani ya nyumba ya mwalimu huyo.
Ama kweli dunia ina mambo, na ukistaajabu ya Mussa kweli utayaona ya Firauni kwa mwalimu huyu wa Sekondari ya Kibasila Jijini Dar es salaam. Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwalimu Gaudensia Missanga mkazi wa Kisiwani kata ya Sandali wilayani Temeke anadaiwa kuishi katika chumba ambacho amehifadhi lundo la kinyesi hali ambayo inatishia usalama wa afya yake. Hebu jenga picha, mwalimu wa shule ya Sekondari halafu anaishi ndani na kinyesi! Hivi hii imekaaje? Mwandishi wa habari hizi amefika hadi kwenye nyumba anayoishi mwalimu huyo anayefundisha masomo ya sayansi na kuzungumza na mwenye nyumba Reuben Shayo ambaye ameeleza kilicho sababisha kubaini uchafu huo.
‘’Tuliona funza wakitoka chini ya mlango wake na harufu mbaya ikitoka na mwenzetu hatujawahi kumuona akioga wala akiingia chooni ndiyo tukabaini hali hii,’’alisema Shayo. Kwa upande wake mwalimu Gaudensia anayetuhumiwa kuishi na kinyesi kinachodhaniwa kuwa ni cha binadamu hakuweza kupatikana kujibu tuhuma hizo na alipopigiwa simu yake ya mkononi ilikuwa inaita bila majibu. Hadi mwandishi wa habari hizi anaondoka nyumbani kwa mwalimu huyo chumba chake kilikuwa kimefungwa huku taratibu zingine zikiwa zinaendelea.

Tuesday, February 24, 2015

HIZI NI NCHI KUMI USIMWACHE MPENZI {wa kike}.......WAKO MWENYEWE

Yako mengi mazuri ya maeneo mbalimbali tunayajua, mfano ni ile list ya Majiji salama zaidi Duniani kwa kuishi, nikakuwekea na ile nyingine ya Beach kali zaidi duniani, leo nimeipata hii nashare na wewe tena mtu wangu.
Gazeti la Daily Mail ni moja ya Magazeti makubwa zaidi Uingereza na Ulaya, wataalamu wao wamefanya utafiti na kuyataja maeneo kumi ambayo siyo salama duniani kwa wanawake kutembelea kwa shughuli yoyote ikiwemo kutalii kama wakiwa peke yao.
India: Jamaa wanasema huku kumekuwa na stori nyingi za matukio ya ubakaji wa wanawake, hii imefanya baadhi ya watalii kuwa na hofu ya kutembelea nchi hiyo. Ripoti hiyo inaonesha kunaripotiwa tukio la ubakaji kila ndani ya dakika ishirini. Brazil: Ripoti inaonesha matukio ya ubakaji, unyanyasaji wa kijinsia, wizi wa kutumia silaha ni tatizo kwa nchi hii. Matukio ya ubakaji yameongezeka kwa 157% kati ya mwaka 2009 na 2012.
Uturuki: Huku nako ishu ni matukio ya ubakaji, yanashika kasi kila siku. Thailand: Ishu kubwa ni unyanyasaji wa kijinsia kwa upande wa huku, dawa za kulevya na pombe zimetajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa.
Egypt: Tokea kumetokea mapinduzi ya utawala 2011 hali haiku sawa bado, unyanyasaji wa kijinsia nako umeshika kasi kubwa. Colombia: Ripoti hiyo inaonesha Polisi wanadili kwa kiasi kidogo sana na ishu ya kulinda wanawake, ni mara chache watuhumiwa wa makosa ya ubakaji wamefikishwa Mahakamani.
South Africa: Hii ni ya kwanza kutajwa kutoka Africa, unyanyasaji wa kijinsia, wizi wa kutumia silaha, na ubakaji ni matatizo makubwa sana kwenye nchi hii.
Morocco: Watalii wa kike wanashauriwa kuvaa kama wenyeji wa nchi hii lakini ishu za ubakaji zinatajwa kwa kiwango cha juu kwa watalii wanawake ambao wanakuwa peke yao.
Mexico: Japo Serikali imeweka nguvu nyingi kuhakikisha tu watalii wanakuwa salama, bado wizi wa kutumia silaha uko kwa hali ya juu sana pamoja na ubakaji wa wanawake kwenye vyombo vya usafiri wengi imewatia hofu.
Kenya: Utalii imekuwa biashara kubwa kwa nchi hii, ripoti hiyo imeitaja kuwa unyanyasaji wa kijinsia uko kwa kiwango kikubwa sana kwa wanawake.
Credit TzA

CHEGE NA KITAMBAA CHEUSI.............!


Picha ya Chege na Temba iliyozagaa mtandaoni yaleta chuki kati ya Chege na Miamartha, baada ya mtangazaji huyo kuweka Instagram picha hiyo iliyozungushiwa alama nyekundu kwenye mkono wa Chege ikionyesha kitambaa cheusi alichokuwa kajifunga na kuuliza kama ni Hirizi.