Subscribe:

Friday, February 27, 2015

UKISTAAJABU YA MUSA UTAONA YA MWALIMU WA SAYANSI ANAYEISHI NA LUNDO LA KINYE NA MIKOJO NDANI YA CHUMBA CHAKE

Kinyesi kilichokutwa ndani ya nyumba ya mwalimu huyo.
Ama kweli dunia ina mambo, na ukistaajabu ya Mussa kweli utayaona ya Firauni kwa mwalimu huyu wa Sekondari ya Kibasila Jijini Dar es salaam. Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwalimu Gaudensia Missanga mkazi wa Kisiwani kata ya Sandali wilayani Temeke anadaiwa kuishi katika chumba ambacho amehifadhi lundo la kinyesi hali ambayo inatishia usalama wa afya yake. Hebu jenga picha, mwalimu wa shule ya Sekondari halafu anaishi ndani na kinyesi! Hivi hii imekaaje? Mwandishi wa habari hizi amefika hadi kwenye nyumba anayoishi mwalimu huyo anayefundisha masomo ya sayansi na kuzungumza na mwenye nyumba Reuben Shayo ambaye ameeleza kilicho sababisha kubaini uchafu huo.
‘’Tuliona funza wakitoka chini ya mlango wake na harufu mbaya ikitoka na mwenzetu hatujawahi kumuona akioga wala akiingia chooni ndiyo tukabaini hali hii,’’alisema Shayo. Kwa upande wake mwalimu Gaudensia anayetuhumiwa kuishi na kinyesi kinachodhaniwa kuwa ni cha binadamu hakuweza kupatikana kujibu tuhuma hizo na alipopigiwa simu yake ya mkononi ilikuwa inaita bila majibu. Hadi mwandishi wa habari hizi anaondoka nyumbani kwa mwalimu huyo chumba chake kilikuwa kimefungwa huku taratibu zingine zikiwa zinaendelea.

Tuesday, February 24, 2015

HIZI NI NCHI KUMI USIMWACHE MPENZI {wa kike}.......WAKO MWENYEWE

Yako mengi mazuri ya maeneo mbalimbali tunayajua, mfano ni ile list ya Majiji salama zaidi Duniani kwa kuishi, nikakuwekea na ile nyingine ya Beach kali zaidi duniani, leo nimeipata hii nashare na wewe tena mtu wangu.
Gazeti la Daily Mail ni moja ya Magazeti makubwa zaidi Uingereza na Ulaya, wataalamu wao wamefanya utafiti na kuyataja maeneo kumi ambayo siyo salama duniani kwa wanawake kutembelea kwa shughuli yoyote ikiwemo kutalii kama wakiwa peke yao.
India: Jamaa wanasema huku kumekuwa na stori nyingi za matukio ya ubakaji wa wanawake, hii imefanya baadhi ya watalii kuwa na hofu ya kutembelea nchi hiyo. Ripoti hiyo inaonesha kunaripotiwa tukio la ubakaji kila ndani ya dakika ishirini. Brazil: Ripoti inaonesha matukio ya ubakaji, unyanyasaji wa kijinsia, wizi wa kutumia silaha ni tatizo kwa nchi hii. Matukio ya ubakaji yameongezeka kwa 157% kati ya mwaka 2009 na 2012.
Uturuki: Huku nako ishu ni matukio ya ubakaji, yanashika kasi kila siku. Thailand: Ishu kubwa ni unyanyasaji wa kijinsia kwa upande wa huku, dawa za kulevya na pombe zimetajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa.
Egypt: Tokea kumetokea mapinduzi ya utawala 2011 hali haiku sawa bado, unyanyasaji wa kijinsia nako umeshika kasi kubwa. Colombia: Ripoti hiyo inaonesha Polisi wanadili kwa kiasi kidogo sana na ishu ya kulinda wanawake, ni mara chache watuhumiwa wa makosa ya ubakaji wamefikishwa Mahakamani.
South Africa: Hii ni ya kwanza kutajwa kutoka Africa, unyanyasaji wa kijinsia, wizi wa kutumia silaha, na ubakaji ni matatizo makubwa sana kwenye nchi hii.
Morocco: Watalii wa kike wanashauriwa kuvaa kama wenyeji wa nchi hii lakini ishu za ubakaji zinatajwa kwa kiwango cha juu kwa watalii wanawake ambao wanakuwa peke yao.
Mexico: Japo Serikali imeweka nguvu nyingi kuhakikisha tu watalii wanakuwa salama, bado wizi wa kutumia silaha uko kwa hali ya juu sana pamoja na ubakaji wa wanawake kwenye vyombo vya usafiri wengi imewatia hofu.
Kenya: Utalii imekuwa biashara kubwa kwa nchi hii, ripoti hiyo imeitaja kuwa unyanyasaji wa kijinsia uko kwa kiwango kikubwa sana kwa wanawake.
Credit TzA

CHEGE NA KITAMBAA CHEUSI.............!


Picha ya Chege na Temba iliyozagaa mtandaoni yaleta chuki kati ya Chege na Miamartha, baada ya mtangazaji huyo kuweka Instagram picha hiyo iliyozungushiwa alama nyekundu kwenye mkono wa Chege ikionyesha kitambaa cheusi alichokuwa kajifunga na kuuliza kama ni Hirizi.

Wednesday, January 7, 2015

Merkel kukutana na Cameron jijini London

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wanatarajiwa leo kuzungumzia mipango ya Cameron kujadili upya uhusiano wa Uingereza na Umoja wa Ulaya. Ziara ya Merkel jijini London ni sehemu ya msururu wa safari katika mataifa kadhaa ya kigeni ili kuyaweka mambo sawa kabla ya mkutano wa kilele wa kundi la mataifa saba yenye nguvu kiuchumi ulimwenguni - G7 ambao atauandaa mnamo Juni 7 na 8 mjini Munich. Merkel na Cameron pia watajadili kuhusu masuala ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili pamoja na sera ya Ulaya ambayo imeuweka uhusiano kati ya viongozi hao wawili kwenye mtihani katika miezi ya karibuni. Masuala hayo ni pamoja na nia ya Cameron kutaka kupunguza idadi ya wahamiaji wanaoingia Uingereza kutokea nchi za Umoja wa Ulaya, hali ambayo amekiri mwezi Novemba kuwa itahitaji kutafakariwa upya mikataba ya Ulaya. Ziara ya Merkel imekuja miezi minne kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu wa Uingereza.

MAZUNGUMZO YA AMANI YAAHIRISHWA HUKO LIBYA

Umoja wa Mataifa umeakhirisha mazungumzo ya amani kati ya pande zinazopigana vita nchini Libya.Wakati huo huo ndege za kivita za serikali ya mjini Tobrouk zimeishambulia meli ya mafuta ya Ugiriki iliyotia nanga Derna [Picha ya mji mkuu wa Libya Tripoli unaodhibitiwa na wafuasi wa itikaadi kali]

Picha ya mji mkuu wa Libya Tripoli unaodhibitiwa na wafuasi wa itikaadi kali
Mazungumzo hayo yalikuwa awali yafanyike Disemba tisaa iliyopita,lakini yaliakhirishwa mara kadhaa kutokana na mapigano kupamba moto kati ya vikosi tiifu kwa serikali inayotambuliwa kimataifa na wanamgambo wanaoungwa mkono na makundi ya itikadi kali. "Mazungumzo yaliyopangwa hayakufanyika" amesema msemaji wa Umoja wa mataifa Stephane Dujarric.Mjumbe wa Umoja wa mataifa Bernardino Leon alizungumza na pande zote ili kusaka ridhaa kuhusu wakati na mahala ya kile kilichokusudiwa kuwa duru ya pili ya mazungumzo kuhusu hali inayozidi kuwa mbaya nchini Libya.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa,Dujarric ametaja "shida zilizojitokeza katika kutafuta "mahala yanayokidhi masharti ya usalama" kuwa ni miongoni mwa sababu za kuakhirishwa mkutano huo. Serikali mbili hasimu na mabunge mawili tofauti yanatawala Libya
[Matangi ya mafuta yafuka moto Sidra]


Matangi ya mafuta yafuka moto Sidra
Miaka zaidi ya mitatu tangu alipong'olewa madarakani na baadae kuuliwa Moammar Ghaddafi katika vuguvugu la mageuzi lililoungwa mkono na nchi za magharibi,Libya ingali bado imezama katika bahari iliyosheheni silaha na makundi ya wanamgambo wenye silaha nzito nzito,na kusimamiwa na serikali mbili na mabunge mawili yanayopingana. Bernardino Leon aliwahi kusimamia duru ya kwanza ya mazungumzo kati ya wabunge wanaohasimiiana katika mji wa Ghadames mwezi septemba uliopita,lakini hakuna matokeo yoyote yaliyopatikana. Juhudi zake za kuitisha duru mpya ya mazungumzo na kuhimiza mazungumzo mengine sambamba kati ya pande zinazohasimiana zimeshindwa hadi sasa licha ya onyo la baraza la usalama la Umoja wa mataifa lililotolewa mwezi octoba mwaka jana kutaka kuwachukulia hatua,watakaotaka kuvuruga juhudi hizo.
Bunge linalotambuliwa kimataifa limepiga kura wiki iliyopita kutohudhuria mazungumzo yoyote ambayo mahasimu wao walioko Tripoli wataalikwa. Majirani wa Libya waitaka jumuia ya kimataifa iingilie kati Öltanker Araevo Archivbild
Meli ya mafuta ya Ugiriki iliyoshambuliwa kwa mizinga na vikosi vya anga vya serikali inayotambuliwa kimataifa Wakati huo huo vikosi vya serikali inayotambuliwa kimataifa yenye makao yake makuu mjini Tobrouk,karibu na mpaka na Misri vimeishambulia meli ya mafuta inayoshikiliwa na wafuasi wa itikadi kali katika bandari ya Derna na kuwauwa mabaharia wawili na wengine kadhaa kujeruhiwa. "Visa kama hivi vinadhihirisha umuhimu kwa pande zote kufikia makubaliano-msemaji wa Umoja wa mataifa Stephane Dujarric amesema. Umoja wa mataifa unasema,tangu mapigano yalipopamba moto,mwezi May mwaka jana,mamia ya raia wa Libya wameuliwa na malaki kuyapa kisogo maskani yao.
Majirani wa Libya wakihofia matumizi ya nguvui yasije yakaenea hadi katika nchi zao,wameitaka jumuia ya kimataifa iingilie kati.Hata hivyo rais Francois Hollande wa Ufaransa amesisitiza uamuzi wowote wa kuingilia kati nchini Libya unabidi upate idhini ya Umoja wa mataifa.

BAHARI YA JAVA NDIPO KULIPOPATKANA MKIA WA NDEGE YA AIR ASIA

Mkia wa ndege ya Air Asia iliyoanguka umepatikana kwenye bahari ya Java, kikosi cha kilichokuwa kikisaka ndege hiyo kimeeleza.
Mkia huo wa ndege hutunza visanduku vyeusi vinavyorekodi mawasiliano ndani ya ndege ambavyo vingeweza kuwasaidia wachunguzi kubaini chanzo cha ajali.

Sehemu hiyo ya mabaki ya ndege ilionekana kwenye eneo la ziada lililoongezwa kwenye operesheni ya kutafuta ndege hiyo. Air Asia ilipotea ilipokuwa ikitoka Surabaya, Indonesia kwenda Singapore tarehe 28 mwezi Desemba ikiwa na Watu 162. Hakuna manusura yeyote aliyepatikana.
Mpaka sasa miili 40 pekee imepatikana lakini Mamlaka zinaamini kuwa abiria wengi zaidi wamenasa ndani ya ndege hiyo.

Tuesday, January 6, 2015

Simu ya mkononi kumaliza Ebola Guinea

Wakati ugonjwa wa Ebola ukiendelea kuwa tishio katika baadhi ya nchi Afrika magharibi, Wataalam wa afya nao wameendelea kuweka jitihada zaidi kuhakikisha kuwa wanaumaliza ugonjwa huo.
Katika jitihada zao hivi sasa wamebuni mpango wa mawasiliano ya simu ya mkononi wenye programu maalum inayotoa taarifa kutoka maeneo yaliyokumbwa na Ebola.

Programu hii ya simu imesambazwa katika maeneo mbalimbali nchini Guinea ambapo ugonjwa huu umesambaa kwa kiasi kikubwa, programu hii huweza kuonesha maeneo ambayo yako hatarini kuathiriwa naVirusi vya Ebola.
Shirika linaloshughulikia idadi ya Watu duniani, UNFPA linatoa elimu kwa wafanyakazi wa jumuia kuhusu namna ya kutumia programu hiyo inayowezesha kushirikisha taarifa kwa kwa wataalamu wa afya katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.
Zaidi ya Watu 1,700 wamepoteza maisha nchini Guinea kutokana na Ebola.
Chanzo BBC

Mwanaume mwenye maumbile ya ajabu

Mwanamume mmoja mwenye uume mbili, amezungumza na BBC kuhusu anavyoiishi na hali yake hio.
Anajulikana tu kama 'Triple D,' na ana umri wa miaka 25 kutoka nchini Mashariki mwa pwani ya Marekani na anadai kuwa amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanawake 1,000.
Mwanamume huyu anaugua ugonjwa ujulikanao kama 'Diphallia' ambapo mwanamume anazaliwa na uume mbili. Kulingana na shirika la kimataifa la afya,BMJ, mwanamume mmoja kati ya milioni tano, duniani huzaliwa na hali hio.
ONYO: Taarifa hii ina lugha ambayo kwa baadhio huenda ikawachukiza
"maisha yangu hayatawahi kuwa sawa tena ikiwa nitajitambulisha kwa dunia nzima, '' alisema Triple D. Hata hivyo BBC ilikubali kubana jina lake na hata kutoonyesha sura yake. Anasema hataki kuwa kichekesho kwa jamii hasa anakoishi.
Katika siku za uchanga wake, wazazi wake walimwambia kutokana na maumbile yake , yeye alikuwa mtoto mwenye maumbile ya kipekee. Anakumbuka wazazi wake wakimketisha chini na kuanza kumuelezea kwamba asidhubutu kucheza mchezo wa 'kalongo' na watoto wenzake na wala asidhubutu kuvua nguo zake za ndani mbele ya watu wengine.

'Mawaidha ya wazazi'
Kutokana na mawaidha ya wazazi wake, aliweza kuweka hali yake kama siri kubwa sana, lakini alipokuwa katika shule ya upili wanafunzi wenzake waligundua siri hio na hapo anasema alipitia masaibu si haba. ''Mwanzoni, sikutaka watoto wengine shuleni kujua hali yangu kwani sikutaka kumuudhi yeyote. ''
Natamani sana wazazi wangu wangeniambia na kunitahadharisha kuwa watu huchekelea kitu wasichokielewa. ''Sikutaka wanaume wenzangu kuhisi vibaya kwamba hawana uume mbili kama mimi na kuanza kunionea kijicho, au kuanzia kunifanyia stihizai na kunichekelea kwamba mimi sio mtu wa kawaida'' alisema 'Triple D'. Alipokua na umri wa miaka 16, alitaka kufanyiwa upasuaji na kuondolewa uume mmoja kwa sababu watu hasa wasichana walianz akunitazama sana katika sehemu yangu ya siri.
''Natamani sana wazazi wangu wangenishauri kuhusu hali yangu basi nisingeopa gata kidogo.''
Alijohiwa kwa nini ni rahisi kwake kuzungumzia hali yake wakati akiendelea kubana jina lake? Alijibu na kusema kila mahali ninapokwenda, kila mtu atanifahamu na kuwa na matarajio makubwa kwangu. Triple D amechapisha kitabu kwa jina: ''Double Header: My Life With Two Penises'', yaani maisha yangu na uume mbili pamoja na anavyokabiliana na hali yake. Anasema sehemu zake hizo zinafanya kazi vyema na kwamba hajabahatika kuwa na uhusiano wa kimapenzi uliodumu kwa mda mrefu.
Kwake changamoto kubwa ni kununua nguo zake za ndani.