Wednesday, January 7, 2015
Merkel kukutana na Cameron jijini London
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wanatarajiwa leo kuzungumzia mipango ya Cameron kujadili upya uhusiano wa Uingereza na Umoja wa Ulaya. Ziara ya Merkel jijini London ni sehemu ya msururu wa safari katika mataifa kadhaa ya kigeni ili kuyaweka mambo sawa kabla ya mkutano wa kilele wa kundi la mataifa saba yenye nguvu kiuchumi ulimwenguni - G7 ambao atauandaa mnamo Juni 7 na 8 mjini Munich. Merkel na Cameron pia watajadili kuhusu masuala ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili pamoja na sera ya Ulaya ambayo imeuweka uhusiano kati ya viongozi hao wawili kwenye mtihani katika miezi ya karibuni. Masuala hayo ni pamoja na nia ya Cameron kutaka kupunguza idadi ya wahamiaji wanaoingia Uingereza kutokea nchi za Umoja wa Ulaya, hali ambayo amekiri mwezi Novemba kuwa itahitaji kutafakariwa upya mikataba ya Ulaya. Ziara ya Merkel imekuja miezi minne kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu wa Uingereza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



0 comments:
Post a Comment